Thursday, April 24, 2014

Waziri Mkuu Malaysia akataa kuthibitisha kama abiria waliokuwa kwenye ndege iliyopotea walifariki.


 


Ni zaidi ya wiki sita sasa baada ya ndege ya Malaysia FH370 kutoweka, waziri mkuu Malaysia amesema serikali yake bado haiko tayari kutangaza kuwa watu 239 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha.
"Kwasasa siko tayari kuzungumzia suala hili nadhani jambo muhimu ni kuheshimu hisia za watu waliopoteza ndugu zao na ukizingatia walishawahi kusema hawatakubaliana na hili mpaka watakapoona ushahidi alisema waziri, Najib Razak.
Hata hivyo, alisema , ni " vigumu kufikiria vinginevyo."
Najib pia aliongeza kuwa serikali yake itatoa reporti ya awali wiki ijayo juu ya kupotea kwa ndege hiyo ambapo tayari ripoti hiyo imeshafikishwa katika Umoja wa Mataifa.
'Mwezi mmoja uliopita, Najib alitangaza kuwa , kwa kuzingatia data zilizopatikana katika satellite ya Inmarsat , wachunguzi walibainisha kuwa kwa mara ya mwisho ndege hiyo ilidondoka katikati ya Bahari ya Hindi, magharibi eneo la Perth na kwamba eneo hilo lipo kijijini na kwa ushahidi huo alisikitika kuwaambia ndugu wa waliopotea kwamba ndege hiyo ilianguka kusini mwa Bahari ya Hindi. '

0 comments:

Post a Comment