Friday, April 18, 2014

Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jna la Joshua Paul (31) mkazi wa kijiji cha Ntokela wilayan Rungwe ameuawa na watu wasiofahamika na kutupwa kwenye shamba la mahindi.



Na mwanafunzi wetu James Mwakyembe



Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Joshua Paul (31) mkazi wa kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe ameuawa na watu wasiofahamika na kutupwa kwenye shamba la mahindi jana jioni.

Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, kamishina mwandamizi wa jeshi la polisi Ahmed Z. Msangi amesema, mwili wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi linalomilikiwa na bwana Yohana Mbilinyi, ukiwa umekatwa kitu chenye ncha kali sehemu ya paji la uso na kifuani. 

Bwana Msangi ameongeza kuwa tayari polisi wanamshikiria Belisi Sikakinda (28) mkazi wa kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe, ambaye alikuwa na marehemu siku ya mwisho, huku uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo ukiendelea kufanyika.

Kamanda Msangi ametoa wito kwa jamii kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwabaini wahusika wa mauaji hayo na sheria ichukue mkondo dhidi yao.

0 comments:

Post a Comment