Sunday, January 12, 2014

Chuo cha Digital Media College of Tanzania-DMCT kufunguliwa jumatano tarehe 15/01/2014


Chuo cha Digital Media College of Tanzania-DMCT kufunguliwa jumatano tarehe 15/01/2014. chuo hiki ambacho kitaanza kutoa kozi mbili kwa ngazi ya cheti kinatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika tanisia ya habari! Katika kuhakikisha utekelezaji wa mabadiliko hayo chuo hiki kitafundisha kozi ya Digital(Online) Journalism pamoja na Radio Production kwa ngazi ya cheti.

Kutokana na wingi wa vyuo vya uandishi wa habari ni dhahiri kwamba wanafunzi wengi wamekuwa wakimaliza masomo na kurudi nyumbani bila mafanikio yoyote ya kupata ajira. Ni jambo la kusikitisha kwa sababu wametumia gharama kupata elimu hiyo ili iwasaidie, lakini pia inasikitisha kukosa kazi wakati habari ni chakula cha kila siku ambacho binadamu anakihitaji bila kushiba! Hakuna mtu anayetosheka na habari, bali kila siku watu wanahitaji habari hivyo mhitimu wa fani ya uandishi wa habari kukosa kazi ni moja ya madhaifu yaliyopo katika vyuo vya uandishi wa habari.

Akielezea Mkurugenzi wa DMCT Bw. Lucas Kulwa alisema kuwa, DMCT imejipanga kuhakikisha kuwa matunda makubwa yanaanza kupatikana mapema kupitia chuo hiki kwa kutoa wanafunzi wenye kiwango cha juu. Aidha katika kuhakikisha hilo, wanafunzi wa DMCT wataanza na kozi ya kiingereza kwa level ya kati ndani ya mwezi mmoja! Akiliendelea kusimulia Bw. Lucas alisema, huwezi kuwa mwandishi wa habari mzuri kama hata kiingereza hujui, dunia ya leo inawasiliana kwa lugha hii ambayo tunaweza kusema ndiyo lugha inayotumiwa na watu wengi duniani.

Hivyo ili uwe mwandishi wa habari mzuri ni lazima ukubali kujifunza na kuongea kiingereza kwa ufasaha! Pia DMCT itatoa kozi ya computer kwa muda wa mwezi mmoja mara tu baada ya kozi ya kiingereza kumalizika. Pia kwakuwa tumenuia kufundisha uandishi wa habari wa kidigitali hatuna budi kuhakikisha wanafunzi wote wanaongea kiingereza na kutumia computer kwa ufasaha!

DMCT itawawezesha wanafunzi wake kuanza kujipatia kipato cha pesa kutokana na kazi za vitendo watakazokuwa wakifanya kama kuandika habari, pamoja na mafunzo ya kumiliki mitandao yatakapofundishwa! Tunatarajia kila mwanafunzi aweze kumiliki blog yake ambayo ataiwekea habari nzuri na zenye tija kila wakati.

Chuo pia kina mikakati mbalimbali kama Tour za nje ya nchi kwenda kujifunza wenzetu wanafanye zaidi. Mtandao huu unakuahidi kuwa utaendelea kukupasha habari mbalimbali kuhusu chuo hiki usikose kuendelea kufuatilia mtandao wetu.







0 comments:

Post a Comment