Friday, April 18, 2014

Polisi mkoani Mbeya wanamshikiria Brown Mensah (25) mkazi wa Songea kwa kumiliki bunduki aina ya gobole na risasi saba za shot gun.



Na mwanafunzi wetu: James Mwakyembe



Polisi  mkoani Mbeya wanamshikiria Brown Mensah (25) mkazi wa Songea kwa kumiliki bunduki aina ya gobole na risasi saba za shot gun.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 12-04-2014 majira ya saa kumi na moja na nusu jioni katika mtaa wa Mwaka-Tunduma kata na tarafa ya Tunduma, wilaya ya Momba mkoa wa Mbeya.

Aidha mtuhumiwa huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi Tunduma na kufanyika upekuzi alikutwa na noti bandia,moja ya  Tshs 10,000/= yenye namba BX-5273247, zingine kumi na saba za Tshs 5,000/= zenye namba AA-08459261 na noti zingine ishirini na tatu za Tshs 2,000/= zenye namba CK-1942911. Taratibu za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinaendelea.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, kamishina mwandamizi wajeshi la  polisi Ahmed Z. Msangi ametoa wito kwa jamii kufuata taratibu za kumiliki silaha.

0 comments:

Post a Comment